Ruzuku za Kujenga Uwezo
Katika kikao cha sheria cha 2022, tuliidhinisha karibu dola milioni $100 za kufanya uwekezaji wa kimkakati ili kuwezesha uthabiti na kupanua utendakazi wa idara ya malezi na elimu ya watoto ya Oregon na kuandaa miundomsingi yetu ili kuwezesha uwekezaji wa shirikisho wa siku zijazo. Kifurushi hiki kinajumuisha Hazina ya Ruzuku ya Kujenga Uwezo wa Watoto (Child Care Capacity Building Grant Fund), ambayo itatoa ufadhili kwa mashirika ya kijamii ambayo yanaweza kushirikiana moja kwa moja na watoa huduma wapya na wa sasa wa huduma za watoto ili kuanzisha vituo vipya vya malezi ya watoto au kupanua vituo vilivyopo ili kuwahudumia watoto zaidi.
Ninaweza kutuma ombi kwa njia gani?
Seeding Justice iko katika mchakato wa kuunda programu ya mtandaoni ambayo itapatikana katika lugha tano zinazozungumzwa zaidi katika jimbo la Oregon. Maombi yatakaguliwa na Kamati ya Uongozi na wafanyakazi wa Seeding Justice, na baada ya Kamati ya Uongozi kuidhinisha au kukataa ombi, waombaji watajulishwa na wafanyakazi wa Seeding Justice.
Usaidizi wa Ziada
Kamati ya Uendeshaji ya Hazina ya Ruzuku ya Kujenga Uwezo wa Watoto pia inapanga kutoa usaidizi unaoendelea wa kufundishana kwa wanafunzi na usaidizi wa kiufundi kwa wapokea ruzuku, ili kuhakikisha kuwa wana fursa za pamoja za kujifunza na kupata usaidizi ili kukabiliana na vikwazo wanapojitahidi kutekeleza au kupanua mipango mpya. Seeding Justice itafanya kazi na wapokea ruzuku kutia saini makubaliano ya ruzuku na kusambaza fedha zilizoidhinishwa, na waombaji wanaweza kustahiki kuingia katika awamu ya ziada ya usaidizi, ikiwa ufadhili utatosha.
Ni nani anayestahiki?
Nyenzo na Rufaa za Malezi ya Watoto
Vituo vya Elimu ya Mapema
Hazina za Pamoja za Usimamizi wa Kazi
Mashirika ya kijamii yenye misingi ya kitamaduni ambayo yana hadhi ya 501(c)(3) au yanafadhiliwa kifedha na mashirika ya 501(c)(3).
Mashirika Mengine ya Kijamii, ikiwa ni pamoja na serikali za Kikabila, taasisi za elimu na wilaya za huduma
Je, fedha zinaweza kutumikaje?
Gharama za kwanza za uendeshaji
Kutengeneza mpango wa biashara wa huduma kwa watoto
Kulipia gharama za miezi 3 hadi 6 ili kusaidia kufikia uwezo wa usajili na kuendeleza gharama za uendeshaji
Kukarabati vituo ili kuweza kupewa leseni ya malezi ya watoto au masharti mengine na/au kuwahudumia watoto zaidi
Usaidizi wa mafunzo ya kitaaluma kwa mafunzo ya lazima au kwa mikataba ya mipango ya ziada ya mafunzo yasiyolipishwa
Vifaa na nyenzo za kuwezesha kufungua au kupanua nafasi
Ruzuku zinaweza kutumika kulipia gharama mbalimbali, kama vile:
Mafunzo ya biashara ya malezi ya watoto
Miradi ya Ukarabati na Mtaji
Kupanua nafasi inayoweza kutumika
Kufanya Matangazo na kutayarisha nyenzo za matangazo
Usaidizi kwa wafanyakazi
Usaidizi wa kupanga na wa kiufundi ili kusaidia kuboresha au kupanua nafasi
Juhudi za kuajiri na kudumisha wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na bonasi, usaidizi wa idara ya rasilimali watu, kushirikiana na mameneja wa ajira, nk.
Pesa hizi zitasimamiwa na Seeding Justice, shirika la kijamii na linaloaminika ambalo lina uzoefu wa kusimamia aina hii ya fedha na kushirikiana na washirika wa jamii. Shirika hili lilichaguliwa kuwa msimamizi wa ruzuku hii kwa sababu linafanya kazi kwenye jamii zilizoathiriwa na zile zilizo karibu zaidi na changamoto husika, ikilinganishwa na mbinu ya kawaida inayotumika zaidi ya juu kwenda chini ya kutuma fedha kwa jamii “maskini”. Wahudumu wake watatumia hekima kuhusu misingi ya ukoo, jinsia na uchumi kuhakikisha fedha hizi zinazifikia jamii na watoa huduma kwa njia ya usawa na bila kuchelewa.
Maamuzi yanafanywaje?
Kama wakala wa kifedha, Seeding Justice pia itasaidia kuandaa kamati ya uongozi inayowajumuisha wadau wa malezi ya watoto katika jamii ili kudhibiti mchakato wa usimamizi na utoaji ruzuku wa hazina. Kamati ya Uongozi itatenga rasilimali kwa ajili ya wafanyakazi wowote wanaohitajika ili kuhakikisha ufikiaji unaofaa, usambazaji wa ruzuku, usaidizi unaoendelea wa kiufundi na usaidizi kwa wapokea ruzuku, n.k. Pia watatoa ripoti za mara kwa mara kwa watunga sheria kuhusu shughuli za hazina, maendeleo na vikwazo tarajiwa.
Mashirika ambayo yatashiriki katika Kamati ya Uongozi ni pamoja na, lakini si tu: